Feminist Studies
MKATABA WA KANUNI ZA UKOMBOZI WA WANAWAKE KIMAPINDUZI KWA WANAHARAKATI WA KIAFRIKA
"Jukwaa maalum la wanaharakati wa ukombozi wa wanawake wa Kiafrika wenye shauku ya kuona kuwepo kwa haki na ukombozi wa wanawake wa Kiafrika lilifanyika katika jiji la Accra, Ghana Novemba 15 - 19, 2006. Jukwaa hilo lilijumuisha pamoja zaidi
ya wanaharakati 100 wa ukombozi wa wanawake wa Kiafrika kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika na hata nje ya bara hili. Mkutano huu uliandaliwa kama nafasi na fursa maalum ya kuwaleta pamojawanaharakati wa ukombozi wa wanawake wa Kiafrika kutoka nyanja na ngazi mbalimbali ukilenga zaidi katika kuwashirikisha wanawake kutoka ngazi za kijamii na wale wa ngazi za kitaaluma kuweza kutafakari kwa pamoja mikakati mbalimbali ya kuwezesha kukuza, kujenga na kuimarisha vuguvugu na nguvu za pamoja za kuleta ukombozi wa wanawake barani Afrika. Pia waliweza
kubuni njia mbalimbali za kuimarisha na kukuza vuguvugu la harakati la ukombozi wa wanawake katika Bara hili."
No Related Publications available